Wazir Junior Apewa Tuzo Ya Mchezaji Bora Mwezi Julai

MSHAMBULIAJI wa Mbao FC ya Mwanza, Waziri Junior amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Julai wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), msimu wa 2019/20.

 

Waziri amewashinda Peter Mapunda wa Mbeya City na Obrey Chirwa wa Azam FC alioingia nao fainali.

Kwenye mechi tano za mwezi Julai, Wazir alitupia jumla ya mabao matano ambayo yaliipa nafasi timu yake kujitoa kwenye nafasi ya 19 iliyokuwa kwa muda mrefu mpaka kufika nafasi ya 16 ikiwa na pointi 45.

 

Nafasi hiyo iliwapa Mbao FC kucheza mchezo wa Playoffs dhidi ya Ihefu ambao waliibuka wababe wa Mbao kwa kuishusha timu hiyo daraja huku Ihefu ikiwa na tiketi ya kushiriki ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

 

Wazir amefunga jumla ya mabao 15 ndani ya Mbao ambapo ana mabao 13 kwenye ligi na mawili kwenye mchezo wa playoffs kwa sasa ni mali ya Yanga akiwa amesaini dili la miaka miwili.Toa comment