Waziri Zungu Mgeni Rasmi Swahili Cup

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa michuano ya Swahili Cup ambapo mshindi wa kwanza anatarajiwa kuondoka na mbuzi.

Akizungumza na mwandishi wetu muandaaji wa mashindano hayo Amiri Auto Accesories amesema lengo la michuano hiyo itakayoshirikisha timu nne ni kuwakutanisha vijana na kubadilishana mawazo.

Amiri alizitaja timu hizo kuwa ni pamoja na Swahili Tyre FC, Vioo FC, Kirambasi FC na Spare Combine ambapo timu hizo zitacheza kwa mtoano.

Amesema mechi ya kwanza itapigwa Agosti 30 mwaka huu kati ya Swahili FC na Kirambasi FC na Septemba 6 mwaka huu itafuatia mechi kati ya Vioo FC na Spare Combine.

Amiri ameendelea kusema katika mechi hizo mshindi wa Agosti 30 na Septemba 6 ndiyo watacheza fainali Septemba 13 ambapo michezo yote  itapigwa Uwanja wa Shule ya Msingi Muhimbili, Upanga Dar.Toa comment