Wema Agoma Kumtusi Zari!

STAA wa Bongo Movies; Wema Isaac Sepetu, amekanusha taarifa kuwa, ameungana na timu ya wazazi wenza wa aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’; Tanasha Donna na Hamisa Mobeto kumtusi Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

 

Wanawake wote hao ni zilipendwa wa Diamond au Mondi kwa nyakati tofauti. Wema ameliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, hakuna kitu kama hicho na wala hana sababu ya kufanya hivyo.

 

“Sijaungana na mtu yeyote kumtusi mtu na sina sababu ya kufanya hivyo. “Mimi siwezi kumtuma mtu kumtusi mtu.

 

“Hakuna mtu yupo kwa ajili ya kumshambulia mtu wala hakuna mtu ameungana kumshambulia mtu,” amesema Wema. Hivi karibuni kumeibuka mashambulizi ya vijembe kati ya Tanasha na Zari, wote wakiwa ni wazazi wenza wa Mondi.

STORI: IMELDA MTEMA, DARToa comment