Wizara ya Afya kuchapisha zabuni zote za Corona – Rais Kenyatta

2 0

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameamuru Wizara ya Afya kuchapisha zabuni zote zinazohusiana na jinsi serikali ilivyoshughulikia janga la Covid-19.

Zabuni zinazotakiwa kuchapishwa ni zile zilizotolewa na mamlaka ya usambazaji vifaa vya matibabu nchini Kenya (Kemsa).

Amri ya rais inafuatia madai ya ubadhilifu wa fedha za umma uliokumba mchakato wa kutolewa kwa zabuni hizo. Wabunge wameanza uchunguzi binafsi kuhusiana na madai hayo.

Afisa mkuu mtendaji wa Kemsa wiki iliyopita alifahamisha kamati ya bunge la seneti kwamba alipokea maelekezo kutoka kwa Waziri wa Afya Mutahi Kagwe na katibu mkuu katika wizara hiyo Susan Mochache kuhusu jinsi ya kutoa zabuni hizo.

Wawili hao wamesema hawajafanya kosa lolote.

“Wizara ya Afya, katika kipindi cha siku 30 zijazo, lazima ibuni njia mwafaka na iliyo wazi itakayoonesha jinsi Kemsa ilivyotangaza na kupeana zabuni hizo,” Rais Kenyatta alisema hayo siku ya Jumatatu wakati alipoongoza kongamano la magavana kuhusu Covid-19.

Posted from

Related Post

Vita ya Viungo Simba vs Yanga

Posted by - January 7, 2020 0
Vita ya Viungo Simba vs Yanga January 7, 2020 by Global Publishers Katika mchezo wa Jumamosi iliyopita  wa Ligi Kuu…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *