Wolper Kutafuta Bwana wa Kumzalisha Gumzo!

PUUZA kejeli zozote za kuenea kwa Virusi vya Corona ambavyo vimekuwa gumzo, lakini kubwa lingine wiki hii lilikuwa ni mwanadada Jacqueline Wolper kutangaza kuwa anatafuta bwana wa kuzaa naye.

 

Wolper alisema anaona ni wakati sahihi sasa umefika wa yeye kuzaa, akaanika na vigezo vya mwanaume anayetaka kuzaa naye. Amesema hataki awe mume wa mtu, asiwe tajiri na awe mchapakazi.

 

“Awe na hofu ya Mungu na asiwe anavuta sigara wala unga, kilevi chochote ruksa. Asiwe staa, kabila na dini yoyote. Awe msafi full time, asiwe na mtoto. Umri miaka 30 na kuendelea…” Amejinadi Wolper kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram.

 

Baada ya kujinadi huko, Wolper alikula matusi ya ‘hela yote’ huko Instagram. Watu walimponda kwa kumuambia amekosa mafunzo, wengine wakasema anajidhalilisha huku wengine wakidai hawamuelewi kwani hivi karibuni tu alijinadi kuwa anatoka na staa wa Hip Hop Bongo, Young Killer.

 

Baada ya kuona ‘wachawi’ wengi kwenye posti hiyo, Wolper alilazimika kuifuta fasta kuepuka kuzidi kula matusi ya nguoni.

 
Toa comment