Yafahamu Mambo makuu 9 ambayo bado hayajafahamika kuhusu Covid-19

13 0

Mtu anahisi ni kana kwamba mlipuko huu umekuwepo kwa muda mrefu, lakini dunia ilitambua uwepo wa virusi vya corona mwezi Disemba. Kicha ya juhusi kubwa za wanasayansi kote duniani, kuna mengi ambayo bado hatujayafahamu, na sote kwa pamoja tumekua ni sehemu ya utafiti unaofanyika katika sayari kujaribu kupata majibu ya kile ambacho hatujakifahamu juu ya coronavirus.

Yafuatayo ni baadhi ya maswali makubwa yanayojitokea

1.Ni watu wangapi ambao wamepata maambukizi?

Ni moja ya maswali ya kimsingi, lakini pia moja ya maswali muhimu

Kuna mamia kwa mamia ya visa vya coronavirus kote duniani, lakini lakini tunachokielewa ni sehemu moja tu ya jumla ya maambukizi. Na idadi tunayopewa kila mara inatukanganywa zaidi n na idadi ambayo haijulikani ya visa vya watu wenye dalili-watu ambao wanavirusi lakini hawahisi kuugua.

Kutengenezwa kwa kipimo cha kinga ya mwili kutawasaidia watafiti kuona ikiwa mtu yeyote amewahi kuwa na virus. Ni wakati huo tututakapoweza kuelewa ni kwa kiwango ngani au ni kwa vipi ni rahisi coronavirus inasambaa.

Lakini je kuna haja ya kutumia barakoa?

2. Hatujafahamu inauwezo wa kuua wa kiasi gani.

Hadi tutakapofahamu ni visa vingapi vimekuwepo, ni vigumu kuelewa ugonjwa huu unaweza kuua kwa kiwango gani. Kwa sasa inakadiriwa kuwa takriba 1% ya watu wanaopata maambukizi wanakufa. Lakini kuna idadi kubwa ya dalili kwa wagonjwa, viwango vya vifo vinaweza kupungua.

3. Idadi kamili ya dalili zake

Dalili kuu za coronavirus ni kiwango cha juu cha joto la mwili, kikohozi na kikavu – hizi ndizo unazopaswa kuziangalia.

Kuvimba koo, maumivu ya kichwa na kuharapia vimekua vikiripotiwa katika baadhi ya visa na kuna tetesi zinazoendelea kuongezeka kuwa mgonjwa kupoteza uwezo wa kutambua harufu ni mojawapo ya athari za virusi hivyo kwa baadhi ya watu.

Lakini swali muhimu zaidi ni ikiwa dalili za mafua za mafua ya kawaida kama vile kutokwa na makamasi au kupiga chafya huwa kwa baadhi ya wagonjwa wa sasa.

Tafiti zimeonyesha kuwa inawezekana kuwa watu wanaweza kuwa na maambukizi ya coronavirus bila wao kujua kuwa wana virusi vya Corona

4. Nafasi ya watoto katika kusambaza virusi.

Watoto wanaweza kupata maambukizi ya coronavirus. Hata hivyo huwa wanapata dalili kidogo na kuna vifo vichache miongoni mwa watoto ikilinganishwa na watu wazima.

Waotot kwa kawaida huwa ni wasambazaji wakuu wa magonjwa, kwa sehemu kubwa kwasababu wanachangamana na watu wengi(hasa katika maeneo yao ya michezo), lakini kwa virusi hivi , haijaelezwa wazi ni kwa kiwangp gani wanasaidia kueneza coronavirus.

5. Ulitoka wapi hasa.

Virusi vilitambuliwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan, Uhina, mwishoni mwa mwaka 2019, ambako kulikua na kisa katika soko la wanyama.

Maafisa rasmi waliita coronavirus, Sars-CoV-2, vina uhusiano wa karibu na virusi ambavyo vinawaathiri popo, hata hivyo inadhaniwa kuwa virusi hivyo vilivyotoka katika popo viliingia kwenye aina nyingine ya kiumbe asiyejulikana ambaye ndiye alivisambaza kwa watu.

“Ukosefu wa maelezo kamili juu ya namna binadamu aliambukizwa “umesalia kuwa kitu kisichofahamika na unaweza kusababisaha maambukizi zaidi.

6. Ikiwa kutakua na visa vichache katika msimu wa joto .

Mafua na homa hushamiri zaidi katika majira ya baridi kuliko majira ya joto, lakini bado haijafahamika ikiwa hali ya hewa ya joto inaweza kuzuia kusambaa kwa virusi

Washauri wa sayansi wa serikali ya Uingereza wameonya kuwa haijawa wazi ikiwa hali ya hewa itaathiri kusambaa kwa virusi .

7. Ni kwanini baadhi ya watu hupata dalili mbaya zaidi kuliko wengine.

Covid-19 ni maambukizi madoko kwa wengi. Hata hivyo takribani 20% hupata dalili kali na kuugua sana. Lakini ni kwanini?

Hali ya mfume wa kinga wa mtu unaonekana kuwa nishemu ya sababu, na kuna labda suala la jeni linaweza kuchangia pia mtu kuugua sana au kutougua sana. Kufahamu hili kunaweza kuwezesha njia za kuzuwia watu kulazimika kufikia kiwango cha kupelekwa katika vyumba vya watu mahututi hospitalini.

Iwapo unahisi hofu ya kuambukizwa virusi vya corona hizi ndio dalili
Image captionIwapo unahisi hofu ya kuambukizwa virusi vya corona hizi ndio dalili

8. Ni kwa kiwango gani kinga ya mwili inadumu, na ikiwa unaweza kupata maambukizi mara mbili.

Kuna tetesi lakini kuna ushahidi mdogo kuhusu ni kwa kiwango gani cha kinga ya mwili mtu alichonacho hawezi ama anaweza kupata virusi

Wagonjwa lazima wawe wamejenga kinga ya mwili ili kuweza kufanikiwa kukabiliana na virusi . Lakini kwa kua virusi hivi vimekuwepo kwa miezi michache tu kuna ukosefu wa data za kipindi kirefu kuvihusu. Tetesi za wagonjwa wanaoambukizwa mara ya pili zinaweza kuwa ni kwasababu huenda hawakupimwa sahihi na kuambiwa kuwa hawana virusi the virus.

Suala la kinga ya mwili ni muhimu kwa ajili ya kuelewa ni nini kitakachotokea baada ya muda mrefu.

9. Ikiwa virusi vitabadilika katika hali nyingine

Virusi hubadilika kila wakati, lakini kubadilika kwa muundo wake wa jeni, hakuleti tofauti yoyote kubwa.

Kwa kawaida, unatarajia virusi kubadilika na kuwa katika hali inayoweza kupunguza hatari yake ya kuua kwa muda mrefu, lakini hili si la uhakika.

Hofu ni kwamba kama virusi vitabadilika katika hali nyingine, basi mfumo wa kinga hauwezi kuvitambua na chanjo yake haiwezi kuwa ya ufanisi (kama ilivyo kwa mafua).

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *