Yanga Kukipiga na KMKM Uwanja wa Azam Complex leo

KIKOSI cha Yanga leo Septemba 30 kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya KMKM ya Zanzibar,utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo wa leo ni maalumu kwa ajili ya kujiweka sawa na mechi za Ligi Kuu Bara zinazoendelea ambapo kwa sasa ligi inaingia mzunguko wa tano.

Mchezo wa Yanga kwa mzunguko wa tano itakutana na Coastal Union ya Juma Mgunda Uwanja wa Mkapa, Oktoba 4 unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku.

Yanga mechi yao iliyopita wametoka kushinda bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri Morogoro wanakutana na Coastal Union iliyotoka kushinda bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania.
Toa comment