Yanga SC Kufutiwa Adhabu na Bodi ya Ligi

ZIKIWA zimepita siku kadhaa baada ya Kamati ya Saa 72 kuiadhibu Yanga kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo ya kutumia chumba kisicho rasmi kubadilishia nguo, Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imesema itawaondolea adhabu hiyo kama ikibainika madai yao yalikuwa sahihi. Yanga katika mchezo dhidi ya Simba uliochezwa Januari

 

4, mwaka huu, haikuingia katika chumba rasmi cha kubadilishia nguo kwa madai ya chumba hicho kuwa na harufu isiyoeleweka, ndipo Kamati ya Kamati ya Saa 72 ikaiadhibu kwa kuitaka kulipa faini ya Sh 200,000.

 

Bodi ya ligi wamefikia hatua hiyo baada ya kocha mpya wa Yanga, Lucy Eymael kuwazuia wachezaji kwa mara nyingine juzi walipokuwa wakicheza dhidi ya Lipuli FC, kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa madai kuwa kulikuwa na harufu ambayo alihisi siyo salama kwa wachezaji wake.

 

Championi Ijumaa lilitamfuta mwenyekiti wa Bodi la Ligi Tanzania Bara, Steven Mnguto ambapo alishangazwa kuwepo kwa madai hayo na kusema kuwa itabidi wasubiri ripoti kutoka kwa kamishina wa mechi ili kuona kama walipata malalamiko hayo.

 

“Nashangaa kuwepo kwa madai hayo tena juu ya kuwepo harufu katika vyumba vya kubadilishia nguo, lakini kama ilivyo kanuni yetu tutasubiri taarifa kutoka kwa kamishina wa mechi kuona ripoti yake ipoje, kwa hiyo kama kutakuwa na ushahidi wa madai hayo basi kwanza tutawafutia adhabu Yanga na kisha kufanya uchunguzi wa nani aliyefanya tukio na kumchukulia hatua zaidi,” alisema Mnguto.
Toa comment