Yanga Wazindua Rasmi Jezi Mpya Msimu wa 2020/201 (Picha+Video)

YANGA kwa kushirikiana na kampuni ya GSM, leo Septemba 11, 2020  wametambulisha jezi rasmi za timu hiyo watakazozitumia msimu wa 2020/21.

Hafla hiyo ya utamburisho wa jezi hizo mpya ilifanyika leo asubuhi Makao Makuu ya timu hiyo Jangwani jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa hizo ndiyo jezi rasmi na halari za Yanga watakazozitumia katika msimu ujao.

Mwakalebela alisema kuwa, jezi hizo zina ubora mkubwa ukilinganisha na jezi za msimu wa 2019/ 20 na amewaomba mashabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga kununua jezi kwenye maduka yatakayotangazwa na Kampuni ya GSM tu na watawachukulia hatua watuwote watakaouza jezi feki.

Pia ametumia muda huo kuwaeleza Mashabiki, Wanachama na Wapenzi wa Yanga kuwa mwaka huu wamesajili vizuri na wana kikosi bora, imara na cha kupambana na timu yoyote, matokeo ya juzi ya sare dhidi ya Tanzania Prisons ni mwanzo tu kuanzia Jumapili hii kitaanza kutoa burudani kwa mashabiki wake. Mashabiki wajitokeze kwa wingi Jumapili Uwanja wa Mkapa kuishangilia timu yao.

Pia wamezindua duka kubwa la vifaa mbalimbali vyenye nembo ya Yanga.

 Toa comment