Yanga yalaani mashabiki wake kuwapiga Simba (+Video)

3 0

Uongozi wa klabu ya Yanga walaani kitendo cha mashabiki wa timu hiyo kuwapiga na kuwafanyia vurugu mashabiki wa Simba ambao walikwenda kuangalia mchezo wa Young Africans dhidi ya Mtibwa Sugar.

 

”Uongozi wa Klabu ya Yanga umesikitishwa na kitendo kisicho cha kiungwana kilichofanywa na baadhi ya mashabiki cha kuwapiga na kuwafanyia vurugu mashabiki wa Simba waliofika kwenye Uwanja wa Jamhuri jana tarehe 27/9/2020 kushuhudia mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.”- Yanga SC

Yanga imeongeza ”Pamoja na kusikitishwa, pia uongozi unalaani vikali tabia hiyo inayo jengeka ya uvunjifu wa amani katika soka na kuviomba vyombo vya Ulinzi na Usalama kuchunguza na hatimaye kuwachukulia hatua za Kisheria wale wote watakao bainika kuhusika na vitendo hivyo.”

”Yanga tunaamini Mpira ni furaha na sio uadui na tunawakumbusha mashabiki wetu kwamba upinzani wetu na Simba unatokana na UTANI WA JADI na siyo uhasama.”

”Aidha uongozi wa Yanga unawashukuru sana Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Morogoro na maeneo mengine waliojitokeza kuiunga mkono timu yao na kufanikisha kupata ushindi katika mchezo huo.”

 

Posted from

Related Post

Video Mpya: Zuchu – Wana

Posted by - April 10, 2020 0
Video Mpya: Zuchu – Wana April 10, 2020 by Global Publishers MTOTO wa Malkia wa Taarab nchini Tanzania, Khadija Kopa,…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *