Yanga Yampiga Chini Cedric Kaze, Kutangaza Kocha Mpya

KLABU ya Yanga imebadilisha uamuzi wa kuendelea na kocha Cedric Kaze ambaye alitarajiwa kuwasili nchini kuungana na miamba hiyo ya soka kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

 

Kaze awali ilisemekana amemalizana na Yanga amekuwa akiripotiwa kuja nchini kuandaa kikosi cha Yanga kwa ajili ya Wiki ya Mwananchi inayofikia kilele Agosti 30, 2020 ambapo watacheza na Aigle Noir ya Burundi katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema Kaze ameomba udhuru wa kuchelewa kuja kutokana na matatizo ya kifamilia.

“Kocha Kaze ametuma ujumbe akiomba wiki tatu zaidi kutokana na matatizo hayo, hivyo uongozi umeona ni vyema utafuta kocha mwingine kutoka kwenye orodha ya waliokuwa wameleta maombi awali haraka iwezekanavyo” imeeleza taarifa hiyoToa comment