Young Killer Aanza Kusaka Mke!

MSANII wa muziki wa Hip Hop Bongo, Erick Msodoki ‘Young Killer’ amesema kwa sasa anatamani kuwa na familia. Akizungumza na Mikito Nusunusu, Young Killer amesema umri wake wa kuoa umefi ka, kilichobaki ni kupata chaguo sahihi.

 

“Kwa sasa naona kama nina umri sahihi kabisa wa kuwa na familia yangu, najua hakuna mwanaume asiyetamani kuishi na mwanamke, hivyo hata mimi natamani sana siku moja nifunge ndoa, pia hapa ninafanya maombi ya kumpata mwanamke ambaye ni sahihi,” alisema Young Killer.

STORI: KHADIJA BAKARI, RISASIToa comment