Young Killer Amponza Wolper

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Erick Msodoki ‘Young Killer’ amemponza staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ambaye amejikuta akioga maneno makali ya kuudhi, RISASI MCHANGANYIKO linakupa mchapo kamili.

 

ILIKUWAJE?

Wikiendi iliyopita kupitia ukurasa wake wa Instagram, Young Killer aliweka picha aliyopiga wakiwa kimahaba na Wolper na kuelezea hisia alizonazo juu ya mrembo huyo.

“Yaani wewe mwanamke usiku silali, mchana tarime, happy women’s day,” aliandika Young Killer.

 

AMPONZA WOLPER

Katika kile kilichoonekana kuwa amemponza Wolper, watu mbalimbali walichukua picha na maneno aliyoandika na kuposti kwenye kurasa zao, ambapo wafuasi wao wengi walianza kumshushia maneno makali mwanadada huyo.

 

Wafuasi hao madai yao makubwa ni kwamba Wolper amekuwa akiwapenda dogodogo (wanaume wadogo kiumri) wakati yeye ni mkubwa kiumri jambo ambalo linasababisha adharaulike.

 

“Yaani dada nilikuwa nakuheshimu sana, lakini kama unatoka na huyu Young Killer ambaye ni mdogo wako kiumri, kwa kweli heshima imeshuka.

“Naona bado Wolper yupo kwenye harakati zake za kutubemendea watoto wetu,” yalisomeka baadhi ya maoni kwenye Instagram.

 

KILLER ANAPIGA ANGA ZA HAWA

Achana na Young Killer, Wolper amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume tofauti wakiwemo wasanii wa Bongo Fleva kama, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ na mwingine ambaye siyo msanii ni Brown.
Toa comment