Zabibu Kiba Aitolea Uvivu ‘Corona’ Ya Mumewe

DADA wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva; Zabibu Kiba, amesema mumewe Abdi Banda hajapata maambukizi ya virusi vya Corona kama maneno yanavyozidi kusambaa mitandaoni.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Zabibu alisema kuwa alishangaa kuona watu wanasema mume wake ana Corona, jambo ambalo si kweli kwa sababu sehemu anayoishi mzazi mwenzake huyo ina baridi, hivyo ndiyo iliyomsababishia mafua na kikohozi.

 

“Mume wangu hana Corona, ila huko South (Afrika) alipo kwa sasa kuna baridi na yeye kwenye baridi ndio huwa anapata mafua na kikohozi, sasa watu walivyoona hivyo ndipo wakasema ana Corona. Nasema hana kwa sababu baada ya watu kusema sana, ilibidi akapime, lakini kwa bahati nzuri majibu yakawa Negative,” alisema Zabibu.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA

 
Toa comment